1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chavez aangushwa katika kura ya maoni.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWJI

Caracas. Wapiga kura nchini Venezuela wametupilia mbali mabadiliko ya katiba katika kura ya maoni ambayo ingempa rais Hugo Chavez haki ya kujenga uchumi wa kisoshalist katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta na kutawala hadi kufa.

Katika matokeo ya mwisho yaliyotolewa na tume ya uchaguzi, kiasi cha zaidi ya asilimia 51 ya wapiga kura wamepinga mapendekezo ya mabadiliko hayo.

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld ameonya dhidi ya mtindo wa mageuzi ya Chavez na kusema kuwa kura hiyo ya maoni ingeweza kusababisha kuporomoka kwa demokrasia nchini humo. Chavez ametishia kusitisha uuzaji wa mafuta nchini Marekani na kuitaifisha kampeni ya mafuta ya Hispania ya Repsol.