1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea wajitayarishe na mateso; Conte

Sekione Kitojo
12 Machi 2018

Kocha wa Chelsea Antonio Conte asema vijana wake wajitayarishe na mateso watakapoingia uwanjani Camp Nou siku ya Jumatano kuwakabili Barcelona

https://p.dw.com/p/2uC8R
Hertha BSC Berlin Italien Antonio Conte
Antonio Conte kocha wa ChelseaPicha: AP

Katika Premier League  nchini  England , kocha Arsene Wenger  anakiri  kwamba  Arsenal  inasumbuka  kuwavutia tena  mashabiki  ambao  wamekasirishwa  baada  ya maelfu  kubakia  nyumbani  licha  ya  ushindi  wa  mabao 3-0 dhidi  ya  Watford jana Jumapili.

Arsenal Coach Arsene Wenger
Kocha wa Arsenal Arsene WengerPicha: Reuters/H. McKay

Arsenal ililaumu kwamba kuanguka  kwa  theluji ndiko kulisbabisha mashabiki  kuwa  wachache  uwanjani  katika  kipigo  chake cha  hivi  karibuni dhidi  ya  Manchester City , lakini kutokujitokeza  tena kwa mashabiki  wengi  dhidi  ya Watford  kunaweza tu kuwekwa pamoja  kwa mchanganyiko wa hasira na kukata tamaa  baada  ya msimu  mwingine  mbaya.

Fußball Champions League FC Chelsea vs FC Barcelona
Wachezaji wa barcelona katika mpambano dhidi ya ChelseaPicha: picture-alliance/empics/N. Potts

Champions League inarejea  tena  uwanjani  wiki  hii , ambapo  Barcelona  na  Manchester United zina  michezo ya  nyumbani  kesho  na  Jumatano dhidi  ya  Chelsea na Sevilla ya  Uhispania. Timu  hizo zinaingia katika mapambano  hayo  ya  mwisho ya timu 16 zilizobakia katika  Champions League zikitaraji  sare katika  mkondo wa  kwanza  ugenini zinaweza  kuwaingiza  katika  robo fainali  ya  michuano  hiyo.

United inaikaribisha  Sevilla kesho Jumanne huku  matokeo ya  mwanzo  yakiwa  0-0, wakati  Barca  inaikaribisha Chelsea  iliyotoka nayo  sare  ya  bao 1-1 uwanjani Stamford Bridge.

Fußball Champions League FC Chelsea vs FC Barcelona
Mchezaji wa Chelsea Willian akishangiria bao dhidi ya ChelseaPicha: picture-alliance/AP Photo/A. Davy

Kocha  wa  Chelsea  Antonio Conte  amesema wachezaji wake  wajitayarishe  kuteseka  dhidi  ya  barcelona siku  ya Jumatano ,iwapo watataka  fursa ya  kuendelea  katika robo  fainali  ya  Champions League.

Bayern Munich inaelekea  Uturuki  siku  ya  Jumatano kupambana  na  Besiktas huku  ikiwa  na  hakika  ya kuendelea  katika  duru  ya  robo  fainali  baada  ya  kupata ushindi  mnono  uwanjani Allianz Arena  wa  mabao 5-0 , wakati  Roma  ikiwa  nyumbani  inapimana  nguvu  na Shakhtar Donetsk ya  Ukraine huku  matokeo  ya  mchezo wa  kwanza  yakiwa  mabao 2-1 kwa  upande  wa  klabu hiyo  ya  Ukraine.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae / rtre / afpe

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman