1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea yaiduwaza Barcelona

19 Aprili 2012

Didier Drogba ndiye aliyekuwa shujaa wakati Chelsea ilipoiduwaza Barcelona kwa kuifunga bao moja kwa sifuri katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa ligi ya Mabingwa Ulaya.

https://p.dw.com/p/14h2c
Chelsea's Didier Drogba reacts after scoring a goal against Barcelona during their Champions League semifinal first leg soccer match at Chelsea's Stamford Bridge stadium in London,Wednesday, April 18, 2012. (Foto:Matt Dunham/AP/dapd)
Champions League Halbfinale FC Chelsea FC BarcelonaPicha: AP

Chelsea walianza mchuano huo wakiwa na lengo la kulipiza kisasi katika kile ambacho mashabiki wao waliona kuwa ni matokeo ya dhulma miaka mitatu iliyopita. Klabu hiyo ya London ililalamika kunyimwa penalty mbili katika mpambano wa mwaka wa 2009 ambapo Andres Iniesta aliivunja moyo ya mashabiki wa Chelsea kwa kufunga bao lililowapa Barca ushindi wa kufuzu katika fainali. Mechi hiyo ilikamilika 1-1 na Barca wakafuzu wka faida ya bao la ugenini.

Lakini katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali uwanjani Sramford Brigde Jumatano usiku, Chelsea iliifunga Barcelona goli moja kwa sifuri na kuwapa mashabiki wake sababu ya kutabasamu. Barcelona kama kawaida iliumiliki mpira na kuihangaisha safu ya ulinzi ya Chelsea, lakini ilikuwa ni timu ya nyumbani iliyokuwa ya kwanza kupata nafasi nzuri na kuitumia vyema.

Mlinda lango wa Chelsea Petr Cech alikuwa na kibarua cha ziada
Mlinda lango wa Chelsea Petr Cech alikuwa na kibarua cha ziadaPicha: picture-alliance/dpa

Barca yamiliki, Chelsea yafunga

Barcelona ilitamba na kupata nafasi za wazi lakini bahati haikusimama na hivyo Didier Drogba akapata nafasi yake ya kufunga bao baada ya kipa wa Chelsea Petr Cech kupiga mpira mrefu ambao ulimpata Lampard ambaye alimsukumia pasi safi Ramires aliyemmulika Drogba ambaye hakuchelewa kutikisa wavu. Bao hilo la dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza ndilo lililowapa Chelsea sababu ya kuwa na usiku wa kukumbuka katika historia yao.

Lakini licha ya kwua Chelsea inaongoza mkondo wa kwanza kwa faiday a goli moja, vijana hao wa Roberto di Matteo wanafahamu kuhusu kibarua kikali watakachokuwa nacho kule Campo Nou Uhispania nyumbani kwa Barcelona wakati wa mechi ya duru ya pili Jumanne wiki ijayo.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman