1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea yataka kufanya kweli Europa League

14 Februari 2013

Chelsea ya Uingereza,inalenga kusahau yaliyopita na kupambana katika kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa ligi ya Ulaya,Europa League, na Liverpool imeeleza wasiwasi wake kuhusu ubaguzi wa rangi inakutana na Zenit.

https://p.dw.com/p/17eED
Handout released by the UEFA shows the new logo of the UEFA Europa League. The UEFA Executive Committee has approved 26 September 2008 the change of name for the UEFA Cup to the UEFA Europa League from 2009/10. The new name heralds major changes to the competition, which will have a new 48-team group stage with centralised marketing of broadcast rights, a presenting sponsor and an official matchball in addition to centralised sponsorship from the knockout stage and a new logo and visual identity according to the news release by the UEFA. EPA/UEFA HANDOUT EDITORIAL USE ONLY / NO SALES +++(c) dpa - Report+++
Europa League LogoPicha: picture-alliance/dpa

Timu tatu za Ujerumani, Borussia Moenchengladbach, VFB Stuttgart na Bayer Leverkusen zitaingia uwanjani pia leo jioni kuwania kufuzu kuingia katika kundi la timu 18 zitakazosalia.

Chelsea imekuwa timu ya kwanza bingwa kutolewa katika awamu ya makundi ya Champions League na inakabiliwa na mpambano katika kundi la timu 32 zilizosalia katika kinyang'anyiro cha ligi ya Ulaya na ina miadi jioni ya leo na Sparta Prague.

LONDON, ENGLAND - DECEMBER 05: Fernando Torres (L) and David Luiz (R) of Chelsea look on during the UEFA Champions League group E match between Chelsea and FC Nordsjaelland at Stamford Bridge on December 5, 2012 in London, England. (Photo by Scott Heavey/Getty Images)
Wachezaji wa Chelsea wakiwa wameduwaa baada ya kuondolewa katika Champions LeaguePicha: Getty Images

Hawataki wachezaji mashoga

Liverpool wako nchini Urusi huku mashabiki wa timu ya Zenit mwezi Desemba walitoa wito kwa klabu yao kutowasajili wachezaji ambao si wazungu na ama ambao ni mashoga, na mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo Ian Ayre amesema katika tovuti ya klabu hiyo kuwa timu yake imeeleza wasi wasi wake katika barua iliyotumwa kwa shirikisho la kandanda barani Ulaya , UEFA na pia klabu ya Zenit St. Petersburg.

Die Mannschaft des FC Liverpool, (hinten l-r) Torwart Pepe Reina, Steve Finnan, Sami Hyypia, Peter Crouch, Jamie Carragher, Ryan Babel, (vorn l-r) Alvaro Arbeloa, Yossi Benayoun, Steven Gerrard, Andrej Woronin, Javier Mascherano, stellt sich am am 15.08.2007 im Hinspiel der 3. Runde der Champions League - Qualifikation in der Begegnung FC Toulouse gegen FC Liverpool im Municipal Stadion in Toulouse, Frankreich zum Mannschaftsfoto auf. Toulouse unterlag mit 0:1. Foto: Photos Davy +++(c) dpa - Report+++
Kikosi cha FC LiverpoolPicha: picture alliance/dpa

"Limekuwa suala kuu la kutia wasi wasi kwetu. Tunasubiri jibu kuhusiana na hilo," amesema.

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers atateremsha uwanjani kikosi madhubuti kabisa mjini St Petersburg, akimwacha kando mchezaji aliyejiunga na kikosi hicho hivi karibuni Daniel Sturridge na Philippe Coutinho, ambao wanafungwa na sheria kutokuwamo katika orodha ya wachezaji wa kikosi hicho.

Nahodha wa Chelsea John Terry amesema kuwa kikosi chake kinaichukulia ligi ya Ulaya kwa dhati hata kama ni kama tukio la ligi ya pili.

England's captain John Terry points during the international friendly soccer match between England and Sweden at Wembley Stadium in London, Tuesday, Nov. 15, 2011. (Foto:Matt Dunham/AP/dapd)
Nahodha wa Chelsea John TerryPicha: dapd

"Hivi sasa tumo katika Ligi ya Ulaya na kuna ujumbe mmoja tu hapa- tunataka kwenda katika ligi hiyo na kushinda . Hilo ndio lengo letu," amesema Terry.

Cech anacheza kwao

Mlinda mlango Petr Cech anacheza nchini mwake na dhidi ya klabu ambayo aliichezea mwaka 2001-02 , na anafahamu kuwa wenyeji watakuwa moto wa kuotea kwa mbali.

"Kwao wao utakuwa mchezo mkubwa mno katika wakati wao, kwa hiyo hiyo ndio hatari kwasababu watataka kuonyesha kuwa wanaweza kufanya vizuri dhidi yetu", amesema Cech, na kuongeza kuwa Sparta ina mchanganyiko mzuri wa vijana , wachezaji wenye uchu na wale wenye uzoefu.

Mabingwa watetezi Atletico Madrid pia wanakabiliwa na upinzani kutoka Urusi, Rubin Kazan, na mlinda mlango wao Sergio Asenjo, ana wasi wasi mkubwa na mshambuliaji mrefu wa Kazan , Jose Rondon.

Mabingwa wa zamani Inter Milan wana miadi na timu kutoka mashariki ya Ulaya , Cluj kutoka Romania.

Timu za Bundesliga

[35505565] SpVgg Greuther Fürth - VfB Stuttgart Fußball Bundesliga 15. Spieltag: SpVgg Greuther Fürth - VfB Stuttgart am 01.12.2012 in der Trolli Arena in Fürth (Bayern). Der Stuttgarter Shinji Okazaki (M) jubelt mit seinen Kollegen über seinen Treffer zum 0:1. Foto: Daniel Karmann/dpa (Achtung Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z. B. via Bilddatenbanken).) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wachezaji wa VfB Stuttgart wakishangiria baoPicha: picture-alliance/dpa

Borussia Moenchengladbach inapambana jioni ya leo na Lazio Rome ambayo itamkosa mshambuliaji wake kutoka Ujerumani Mil´roslav Klose, pamoja na nahodha Stefano Mauri.

Hannover 96 inakutana na kikosi kinachoongozwa na mshambuliaji kutoka Cameroon , Eto'o , VFB Stuttgart ina kabiliana na Genk ya Ubeljigi wakati Bayer Leverkusen inaikaribisha Benfica Lisbon ya Ureno.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Josephat Charo