1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Afrika

Ute Schäfer9 Februari 2007

Ziara ya rais wa China Hu Jintao barani Afrika imeongoza kwa baadhi ya nchi za ulaya kuzionya nchi za kiafrika zichunge na hatari za ukoloni mpya.Uchambuzi wa Ute Schäfer,mkuu wa Idhaa ya Afrika:

https://p.dw.com/p/CHKU

Rais wa Jamhuri ya watu wa China Hu Jintao baada ya kuzuru jana Msumbiji, atakamilisha ziara yake ya mataifa 8 ya Afrika visiwani Seyschelles.Ziara hii imezusha hofu na wasi wasi barani Ulaya na katika kambi ya magharibi kwa jumla.

Ulaya inachukulia mambo rahisi.Wakiitupia jicho ziara ya rais wa China Hu Jintao barani Afrika mjini Brussels (makao makuu ya UU) na serikali ya Ujerumani mjini Berlin inazungumzwa hiki ni kitisho kipya cha ukoloni kwa bara la afrika.

Kuangalia mambo hivyo ni kuufumbia macho ukweli wa mambo na wakati huo huo kunatoa hoja na sababu nyingi kwanini China wakati huu imeshika usukani barani humo na sio bara la Ulaya.

Mafanikio ya China yabaimnisha HASA jambo moja.

Ulaya imepoteza nafasi nyingi ilizopata barani Afrika kushindwa kuzitumia ipasavyo.Dala bilioni kadhaa zimemiminwa katika nchi changa za Afrika ,lakini masikini Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, wanazidi ufukara.Kinyume ifanyavyo China.Baada ya kumalizika enzi ya vita baridi,Ulaya haikuonesha tena hamu ya kisiasa na Afrika.

Ulaya ikaanza kujishughulisha na kupanua umoja wake na sera zake za nje na za misaada ya maendeleo ikazielekea Ulaya ya Mashariki nay a kusini.

Sera za kukuza biashara na bara la Afrika zikapewa kisogo.Msaada wazi wa kiifedha na wa kisiasa kwa nchi za kiafrika zilizoamua kufanya mageuzi haukutolewa. Nchi za Ulaya zikawa “maneno mengi na hakuna vitendo”.Na hayo ndio maoni ya waafrika wengi.

China kinyume chake, inawajengea waafrika mahospitali,madaraja,barabara,inawapatia mipango isio na gharama kubwa ya kupiga vita malaria na maradhi mengine yanayolisibu bara la Afrika…..

Kilichopelekea hali hii kukubalika china Afrika ni kuwa China na Afrika zina masilahi yanayoshabihiana tangu kisiasa hata kiuchumi.Rais wa China Hu Jintao amewaahidi waafrika kuwatetea barabara zaidi katika UM.Kwa njia hii Afrika na china zinavuta kamba upande mmoja linapokuja swali ka kufunguliwa milango ya masoko ya Ulaya kwa bidhaa zao . Usuhuba huu wa kusini na mashariki-South-East Alliance- unaweza katika biashara ya dunia miaka michache tu ijayo ukapalilia upepo mpya.

Kwani,kwa kadri idadi ya wakaazi barani Afrika inavyoongezeka pamoja na China na uchumi wake unaweza kuchangia kuufanya huo uitwao “Ulimwengu wa kwanza I” uanze kuzitia kweli maanani shemu hizo kama washirika wao.

China na Afrika -siusuhuba wa kimapenzi, bali wa kimasilahi na hii wametambua zamani waafrika.Bara la Ulaya kwahivyo, halina haja ya kuilinda Afrika iepukane na hatari kutoka china kama baadhi ya wahariri na wachambuzi wa kisiasa wsemavyo.

China inajitembeza na miongoni mwa viongozi wengi waliosisitiza hayo ni rais wa Ghana,John Kufuor, karibuni kwamba wanaelewa pia hatari ziliopo.Hatari hizo zinaonekana wazi.

Kwa desturi, China inauza n’gambo viwanda vyake pamoja na watumisbhi wake.

Nchini Ghana wafanyikazi wa kichina hawagharimu fedha nyingi kama wenye nchini.

Urari wa biashara kwa sehemu kubwa kama ilivyo nchini Afrika kusini na China, ni wa nafuu kwa China.Na nchini Zambia, karibuni hivi wafanyikazi wa kiafrika wakilalamika kwenye migodi ya shaba kwa ujira mdogo walipwao na masharti ya kazi yasiowaridhisha.