1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Urussi zalaani mipango ya Marekani ya makombora ya ulinzi

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E53a

BEIJING

China na Urussi hii leo zimelaani mipango ya Marekani ya kuweka mfumo wa ulinzi wa makombora katika eneo la ulaya mashariki.Nchi hizo mbili zimetoa taarifa ya pamoja inayosema kwamba mipango hiyo ya Marekani haitasaidia katika suala la amani na pia itavuruga juhudi za kimataifa za kudhibiti silaha pamoja na mpango mzima wa kuzuia uenejazi wa silaha. Marekani inasema kwamba mpango wake wa kuweka makombora ya ulinzi katika baadhi ya nchi za ulaya mashariki una azma ya kuulinda usalama wa washirika wake katika eneo hilo.

Rais mpya wa Urusi Dmitry Medvedev ambaye ameanza ziara yake ya siku mbili nchini China na mwenyeji wake Hu Jintao wametoa taarifa hiyo mjini Beijing.Ziara hiyo ya Medvedev inalengo la kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kibiashara kati ya China na Urussi.Urussi na China zote wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa zimeongeza ushirikiano wao katika sera za nje kwa lengo la kuupunguza ushawishi wa Marekani na kuimarisha uhusiano wa kibiashara.Aidha nchi hizo mbili zinatazamiwa kutiliana saini ushirikiano wa kujenga kinu cha kinuklia utakaogharimu mabillioni ya dolla.