1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaionya Marekani kuhusu Korea kaskazini

Sekione Kitojo
15 Aprili 2017

China imetoa onyo kali jana Ijumaa (14.04.2017)kwamba mzozo kuhusu Korea kaskazini unaweza kuzuka wakati wowote, wakati Pyongyang ikiapa kujibu bila huruma iwapo Marekani itachukua hatua yoyote ya kijeshi. 

https://p.dw.com/p/2bGFB
Nordkorea Machthaber Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un akiwa pamoja na wanajeshi wa nchi hiyoPicha: Getty Images/AFP

Korea  ya  kaskazini  imeionya  Marekani  kuacha  mhemko wake wa  kijeshi  ama  itakabiliwa  na  hatua  ya  kujibu  mashambulizi wakati  kundi  la meli zilizobebeba ndege  za  kivita  zikielekea  katika eneo  hilo huku  kukiwa  na  hofu  kwamba  Korea  kaskazini  huenda ikafanya  jaribio  lake  la  sita  la  silaha  za  kinyuklia.

Mamia  ya  magari  ya  kijeshi  yaliyobeba  watu  ambao  walikuwa wakiimba  na  kushangiria  wakielekea  katika  gwaride  la kuadhimisha  mwaka  wa  105 wa  kuzaliwa  kwa  muasisi  wa  taifa hilo , sherehe  ambazo  zinaingiliana  na  kitisho  cha  hivi  karibuni kabisa  cha  taifa  hilo  lenye  uficho  dhidi  ya  Marekani  na  rais Donald  Trump.

Nordkorea Machthaber Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong UnPicha: picture-alliance/AP Images/W. Maye-E

Wasi  wasi  umeongezeka   tangu  jeshi  la  majini  la  Marekani kuishambulia  Syria  katika  kituo  cha  jeshi  la  anga  kwa makombora  59  chapa  Tomahawk wiki  iliyopita  kujibu shambulio baya  ya  gesi  ya  sumu. Hatua  hiyo  imezusha  maswali  kuhusiana na  mipango  ya  rais  Trump  kwa  Korea  kaskazini , ambayo imefanya  majaribio  ya  makombora  na   nyuklia ikikaidi  vikwazo vya  Umoja  wa  mataifa na  nchi  binafsi.

Syrien USA Luftangriff auf Militärbasis
Meli ya kijeshi ya Marekani USS PorterPicha: picture-alliance/AP Photo/US Navy/F. Williams

Marekani itashindwa 

"Hatua zozote za  uchokozi zinazofanywa  na  Marekani  katika nyanja  za  siasa , kiuchumi  na  kijeshi  ikifuata  sera  zake  za uadui  kuelekea  Korea  kaskazini  zitashindwa  kwa  hatua  kali zitakazochukuliwa  na  jeshi  na  watu  wa   Korea  kaskazini," shirika la  habari  la  Korea  kaskazini  KCNA limesema, likinukuu msemaji wa  mnadhimu  mkuu  wa  jeshi  la   wananchi  wa  Korea.

"Hatua  yetu  kali  ya  kujibu  mashambulizi  dhidi  ya  Marekani  na meli  zake  za  kivita  zitachukuliwa  kwa  njia  ambayo  hakutakuwa na  huruma  na  bila  kumpa  nafasi  mchokozi  kunusurika."

Imesema mhemko  wa  "dhati  wa  kijeshi  wa  utawala  wa  rais Trump, umefikia  katika  awamu  hatari  amayo  haiwezi  kamwe kupuuziwa."

USA Statement Donald Trump zum Luftangriff auf Syrien
Rais Donald Trump wa MarekaniPicha: Reuters/C. Barria

Makamu wa  rais wa Marekani  kwenda Korea

Marekani  imeonya  kwamba  sera  za  uvumilivu  wa  kimkakati kuelekea  Korea  kaskazini  zimefikia  mwisho. Makamu  wa  rais  wa Marekani  Mike Pence  anasafiri  kwenda  Korea  kusini  kesho Jumapili(16.04.2017) katika  ziara  ndefu  ya  siku  10  katika mataifa  ya  Asia.

China, mshirika  pekee  mkubwa  wa  Korea  kaskazini na  ambayo ni  nchi  jirani  hata  hivyo inapinga  mpango  wake  wa  silaha , jana Ijumaa  kwa  mara  nyingine  tenma  imetoa  wito  wa  mazungumzo ili  kutuliza  mzozo  huo.

China PK französischer Außenminister Jean-Marc Ayrault und Wang Yi in Beijing
Waziri wa mambo ya kigeni wa China Wang YiPicha: Reuters/J. Lee

"tunazitaka  pande  zote  kujizuwia  na  uchokozi  na  kutishiana, iwapo  ni  kwa  maneno  ama  vitendo, na  kutoifanya  hali  hiyo kuingia  katika  hatua  ambayo  haitaweza  kubadilishwa  na kushughulikiwa," waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  China  Wang Yi amewaambia  waandishi  habari mjini Beijing.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Sudi Mnette