1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaitaka Iran irudi kwenye mazungumzo

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuGO

China imeitolea mwito Iran ianze tena mazungumzo na jumuiya ya kimataifa. Vyombo vya habari vya China vimemnukulu waziri wa mashauri ya kigeni wa China, Yang Jiechi, akisema swala la nyuklia la Iran limefikia hatua muhimu.

Yang aliyasema hayo wakati wa mazungumzo yake na mpatanishi mkuu wa Iran katika mzozo wa nyuklia, Saeed Jalili, ambaye yumo ziarani mjini Beijing. Inasemekana Jalili anajaribu kutafuta msaada wa China ili kuzuia azimio lengine la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.

Marekani inashinikiza azimio lengine dhidi ya Iran ili ikomeshe urutubishaji wa madiniy a uraniaum.