1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yakosoa malengo ya nchi tajiri huko Copenhagen

9 Desemba 2009

China yasema malengo ya nchi tajiri duniani, kuhusu hali ya hewa hayawezi kuafikiwa.

https://p.dw.com/p/Kxn4
Rais Hu Jintao wa China.Picha: AP

China ambayo inaongoza kwa kutoa viwango vya juu vya gesi inayochafua mazingira, imezishtumu nchi tajiri duniani ambazo pia zinatoa viwango vya juu vya gesi hiyo, kwa kuweka malengo makubwa yasiyoweza kuafikiwa ya kupunguza utoaji huo wa gesi, katika mkutano unaoendelea wa hali ya hewa mjini Copenhagen.

Mpatanishi wa China, katika mkutano huo wa Umoja wa Mataifa, Su Wei alisema malengo waliyojiwekea Umoja wa Ulaya, hayatoshi, na kwamba dhamira ya Marekani pia haiko wazi. Shutuma hizi kutoka China zinakuja wakati, shirika la utabiri wa hali ya hewa ulimwenguni, limetangaza karne iliyopita ndiyo, karne imerekodi viwango vya juu zaidi vya ujoto.

Afisa mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya hali ya hewa, Yvo de Boer katika hotuba yake ya ufunguzi aliwaambia wajumbe, mkutano wa Copenhagen utaweka historia, lakini lazima iwe historia ifaayo.

Mkutano huo ulioanza mapema wiki hii, unalenga kupata makubaliano yatakayochukua nafasi ya mkataba wa Kyoto, pamoja na kupata maafikiano ya uhakika ya kupambana na ongezeko la ujoto duniani.