1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaonya itachukua hatua kali dhidi ya waandamanaji

15 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DOsj

LHASA:

Maafisa wa Kichina wameonya kuwa watachukua hatua kali dhidi ya wapinzani wa serikali wanaoandamana Tibet. Mwenyekiti wa serikali ya Tibet amewatuhumu wanaharakati hao kuwa wanataka kusababisha mtengano wa taifa na akasisitiza hatua kali zitachukuliwa.Vile vile amemlaumu kiongozi wa kidini wa Tibet,Dalai Lama kwa maandamano hayo,madai yaliyopingwa na kiongozi huyo wa kidini.

Kwa mujibu wa ripoti za mashahidi,vifaru vimeingia mji mkuu Lhasa na sehemu ya mji huo umezingirwa.Vile vile hakuna njia ya kuwasiliana kwa simu za mkono.Wakati huo huo Shirika la habari la China Xinhua limethibitisha kuwa watu 10 wameuawa katika mapambano na polisi.