1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yasherehekea leo mwaka kabla Olimpik

Ramadhan Ali8 Agosti 2007

Ilikua shamra shamra mjini Beijing.Wageni 10.000 walikusanyika katika Tianamen Square kushuhudia rais wa IOC akitoa mialiko rasmi kwa nchi 205 kutuma wanariadha wao Beijing 2008 siku kama leo.

https://p.dw.com/p/CHbO

Fashfashi,ngoma za kuigiza za simba na Mialiko ya Halmashauri Kuu ya olimpik Ulimwenguni kwa nchi 205 ambayo ni rekodi kuhudhuria michezo ya 29 ya Olimpik ya kisasa,ni kilele cha sherehe za leo mjini Beijing kuadhimisha mwaka kabla michezo hiyokuanza August, 8 –siku kama leo mwaka ujao:

Rais wa halmashauri kuu ya olimpik Ulimwenguni mbelgiji Jacques Rogge alitoa rasmi mialiko kwa kamati 205 za olimpik ulimwenguni kutuma wanariadha wao wake kwa waume mjini Beijing hapo mwakani.

Akatangaza katika uwanja wa Tianamen Square:

“Ulimwengu unaikodolea macho China na mji wa Beijing kwa matumaini makuu”.

Rogge aliwaambia wageni 10.000 katika sherehe ilioneshwa moja kwa moja na kituo cha TV cha China kutoka uwanja huo.

Akaongeza kusema kwamba, kamati ya maandalio ya olimpik ya jiji la Beijing imefanya kazi kwa bidii sana kuupa mji huo sura ya kiolimpik.Akangeza kusema kwamba, viwanja vya michezo takriban vimekamilika na vinapendeza ajabu.

Wu Bangguo, makamo wa mwenyekiti katika chama cha kikoministi cha china ,alisema China ikitumai kuonesha mfululizo moyo wa kiolimpik.

Shamra shamra za leo katika uwanja wa Tianamen Square, zilianza kwa nyimbo na ngoma kwenye jukwa maalumu lililojemngwa katika kitovu cha uwanja huo.Miongoni mwa waimbaji ni mwanasanaa m ashuhuri wa Hong Kong Andy Lau alieimba “kila mmoja nambari 1.”-Every one is no.one.

Maalfu ya watu wa kawaida walijipanga mistari tangu adhuhuri ya leo kushuhudia burdani hiyo na kuziba njia zote kuelekea uwanja huo.

Imepangwa kwamba sherehe za ufunguzi za michezo ya 29 ya olimpik hapo mwakani zitaanza 2 jioni August 8, 2008.Tarehe 8 mwezi wa 8 2008, imechaguliwa makusudi kwavile nambari 8 ni tarkimu ya bahati nchini China na inalingana na neon la kichina lenye maana ya afya na uzima.Baada ya hotuba za rais wa Halmashauri kuu ya olimpik IOC na viongozi wa China, vinajana walifanya gwaride uwanjani wakibeba bendere za nchi 205 zanachama wa Olimpik.

Michezo hii ni kuwasilisha Olimpik kwa 1/5 ya walimwengu-alisema rais wa IOC Jacques Rogge.

Hapo kabla,rais wa IOC alisdema kuwa kuchafuka kwa hali ya hewa nchini China kunaweza kukalazimisha baadhi ya michezo na hasa ile inayohitaji uvumilivu kama vile mbio za masafa marefu –mbio za baiskeli na marathon kucheleweshwa au kuahirishwa.

Mji wa Beijing unaandaa mashindano 2 ya majaribio wiki hii- mashindano ya 2007 ya ubingwa wa kupiga masikia ulimwenguni-world Rowing junior championships nay ale ya hoki ulimwenguni.