1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchumi wa China wapungua kasi lakini misingi ni imara

Admin.WagnerD19 Januari 2016

China hauikuweza kuyafikia malengo yake ya kiuchumi katika mwaka uliopita kutokana na uchumi wake kustawi kwa asilimia 6.9 Kiwango hicho ni cha chini kabisa katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.

https://p.dw.com/p/1Hfpf
Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: Reuters/A. Song

Takwimu rasmi zilizotolewa leo zimethibitisha kwamba China haikulifikia lengo la ustawi wa asilimia 7 lililowekwa na serikali ya nchi hiyo mwaka uliopita. Hata hivyo uchumi wa nchi hiyo ulistawi kwa asilimia 6.9

Uchumi wa China ulikuwa imara zaidi katika miaka ya hadi hivi karibuni lakini ulianza kukabiliwa na upungufu katika mauzo ya nje,kuzorota kwa vitega uchumi na madeni ya viwango vya juu. Hali ya uchumi wa China ambayo ni nchi ya pili katika nguvu za kiuchumi duniani, inasababisha wasi wasi miongoni mwa wawekaji vitega uchumi wa kimataifa.

Hali hiyo inatokana na mabadiliko ambayo China inayafanya katika muundo wake wa uchumi. Viongozi wa nchi hiyo wanataka China iondokane na kutegemea uuzaji wa bidhaa nje na badala yake uchumi wa nchi hiyo utegmee utashi wa ndani.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wamesema takwimu ziliztolewa leo zimeonyesha matumaini makubwa kuliko hali ilivyo. Profesa wa masuala ya uchumi Hu Xingdou amesema hakuna tofauti kubwa baina asilimia 6.9 na asilimia 7 .

Misingi ya uchumi bado ni imara

Rais Xi wa China Jinping amesema misingi ya muda mrefu ya kiuchumi ya China bado ni imara licha ya kupungua kasi ya ustawi na licha ya ugeu geu kwenye masoko.

Duka kubwa la mahitaji katika mji wa Zhuji
Duka kubwa la mahitaji katika mji wa ZhujiPicha: picture-alliance/dpa/Chinafotopress

Ili kukabiliana na hali hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha uchumi kwenye chuo kikuu cha Peking, Liu Yuanchun ameitaka serikali ichukue hatua za kuuweka sawa mfumo wa fedha na pia amewataka viongozi wa China waache kujiingiza sana katika shughuli za kichumi.

Mtaalamu mwengine ,Enzio Von Pfeil ameishauri China kuondokana na sarafu yake ya Renminbi na hivyo kuwezesha fedha kutolewa kwa urahisi. Mtaalamu huyo pia ameitaka China ianze mpango kamambe wa kutumia fedha kwa sababu serikali bado inayo mawezekano ya kuingilia kati katika harakati za kiuchumi . Amesema serikali inaweza kuekeza katika ujenzi wa miundombinu,kama barabara na madaraja.

Mwandishi:Mtullya Abdu.

Mhariri:Abdul-Rahman