1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chirac chini ya uchunguzi.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ6K

Paris. Majaji nchini Ufaransa wamemuweka rais wa zamani nchini humo Jacques Chirac chini ya uchunguzi rasmi kwa ubadhirifu wa fedha za umma wakati alipokuwa meya wa mji wa Paris. Chirac amepoteza kinga yake ya kutoshtakiwa baada ya kuondoka katika madaraka ya urais May mwaka huu. Wakili wa Chirac amesema kuwa uchunguzi unalenga kuhusu kazi ambazo zinadaiwa zilitolewa watu wa mrengo wa kulia ambao walikuwa wanamuunga mkono wakati wa utawala wa Chirac kama Meya kati ya mwaka 1977 na 1995. Chirac amekuwa kila mara akikanusha madai hayo.