1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chissano azawadiwa tuzo ya Mo Ibrahim

22 Oktoba 2007

Taasisi ya Mo Ibrahim imemtunukia tuzo maalum yenye thamani ya dola milioni tano aliyekuwa rais wa Msumbiji Joaquim Chissano.

https://p.dw.com/p/C77b
Joachim Chissano wa Msumbiji ametunukiwa tuzo na Taasisi ya Mo Ibrahim
Joachim Chissano wa Msumbiji ametunukiwa tuzo na Taasisi ya Mo IbrahimPicha: AP

Kamati hiyo ya tuzo inayoongozwa na katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan imeutambua mchango mkubwa wa kiongozi huyo wa zamani.

Licha ya zawadi hiyo ya dola milioni tano kwa mshindi pia kuna zawadi ya doka laki mbili kwa muda wa miaka kumi mfululizo amabzo mshindi atazitunikia miradi mbali mbali ya maendeleo nchini mwake.

Zainab Aziz alizungumza na Dr.Salim Ahmed Salim ambaye ni mmoja wa wanakamati wa taasisi ya Mo Ibrahim na kwanza anaelezea kilichozingatiwa na vigezo vilivyotumika kumteua mshindi.

Uteuzi wa rais mstaafu Chissano umepongezwa pia na wasomi mbali mbali mmoja wapo ni Profesa Mwesiga Baregu, muadhiri muandamizi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kitivo cha siasa.