1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Christopher Mtikila atangaza kuwania mgombea binafsi wa Urais Tanzania

3 Machi 2010

<p>Nchini Tanzania joto la uchaguzi linazidi kupamba moto wakati ambapo shughuli hiyo inasubiriwa kufanyika ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

https://p.dw.com/p/MIZo
Tanzania wajitayarisha na uchaguzi Oktoba 2010Picha: DW
Wagombea wamekuwa wakijiandaa kwa uchaguzi huo na hata chama kipya cha jamii kimepata usajili wa muda mwanzoni mwa wiki hii. Kwa upande mwengine, suala la kuruhusiwa mgombea binafsi kushiriki katika uchaguzi mkuu bado linaendelea kuzusha mitazamo tofauti. Kutokana na hilo, Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia, Christopher Mtikila, ametangaza kuwa hata chama chake kisipomteua kuwawakilisha katika uchaguzi, yeye atawania wadhifa wa rais kama mgombea binafsi. Atafanikiwa? Mwandishi wetu wa Dar es salaam, Christopher Buke, alikutana na Christopher Mtikila na haya ndiyo aliyomulezea

Mwandishi: Thelma Mwadzaya

Mhariri: Othman Miraji