1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chuki dhidi ya wageni ni ujinga

22 Septemba 2016

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha leo (22.09.2016)na ripoti ya serikali kuhusu Umoja wa Wajerumani na kupinga chuki dhidi ya wageni. Mvutano wa Marekani na Urusi Syria pia umegusiwa na wahariri hao.

https://p.dw.com/p/1K6X7
Berlin Modell des geplanten Einheitsdenkmals - Einheitswippe
Eneo la kuonesha Umoja wa Wajerumani mjini BerlinPicha: picture-alliance/dpa/Foto: Milla&Partner

Gazeti la Koelner Stadt - Anzeiger kuhusu ripoti ya serikali inayohusu umoja wa Wajerumani limeandika:

Kupinga ama kukataa kila kitu kuhusu wageni tayari hali hiyo imejikita katika maisha ya watu, hali ambayo ilibadilika kwa kiasi kikubwa katika mwaka 1989. Hali ya mabadiliko na kuingia katika kuchoka inahitaji kufuatiliwa kwa karibu. Ujumbe mmoja lakini hauwezi kupita bila ya kuangaliwa kwa kina. Yule anayeridhia chuki dhidi ya wageni ama kutumia hali hiyo kutoa ghadhabu zake, anajiingiza katika hali ya kutokuwa na ubinadamu na pia anajitumbukiza katika matatizo makubwa. Mhariri anauliza , nani anaweza kupuuzia uwekezaji kutoka nje , wakati dunia inapaswa fungua mipango yake? Chuki dhidi ya wageni sio tu ni ujinga , lakini pia ni ghali.

Gazeti la Westfälische Nachrichten , kutoka Muenster kuhusu mada hiyo linaandika:

Kupambana na vikundi vya watu wenye vipara kutoka mataifa ya kigeni , mashambulizi dhidi ya makambi ya wakimbizi na matusi kutoka kwa wanasiasa, ni hali ambayo inaeleza kwa bahati mbaya hali halisi miaka 26 baada ya muungano wa nchi mbili za Ujerumani.

Lakini kabla ya kunyooshea kidole mpaka wa zamani baina ya upande wa mashariki kwamba ni wabaguzi na upande wa magharibi kwamba wanafuata demokrasia , ni lazima kwanza tukumbuke kuhusu maendeleo yaliyopigwa ya kijamii , kiuchumi na kisiasa katika miongo iliyopita.

Kumekuwa na hali ya udikteta kwa miaka mingi, kwanza wa Wanazi na kisha ukomunist, na hali hii imebakia vichwani mwa watu na maisha ya demokrasia na utamaduni wa maadili ya kijamii hayajaleta tija kabisa.

Upande wa magharibi haujaishi katika maisha haya kabisa tangu mwaka 1945.

Gazeti la Saarbrücker Zeitung , linaandika kuhusu hali ya chuki dhidi ya wageni upande wa mashariki kwamba:

Wengi wa wananchi hasa huko upande wa mashariki hawaelewi nini maana ya demokrasia ama vipi wanaweza kuwachukulia watu kutoka nje. Hawapaswi kuyachafua mafanikio yaliyopatikana katika ujenzi mpya wa eneo la mashariki kutokana na matendo ya watu wachache. Kunahitajika ujasiri mkubwa na nguvu za wananchi kupambana na hali hiyo. Hata hivyo tamko la wazi la serikali ni ishara muhimu.

Syrien Angriff auf Hilfskonvoi
Shambulio dhidi ya msafara wa malori ya misaada nchini SyriaPicha: Getty Images/AFP/O. Haj Kadour

Kuhusiana na suala la hali nchini Syria , gazeti la Nürnberger Nachrichten limeandika:

Iwapo wito wa rais Barack Obama katika hotuba yake katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa ulikuwa na lengo la kuimarisha uhusiano wa kweli kimataifa , ingekuwa ni urithi wa maana sana , na njia ya kutafuta kurejea katika meza ya majadiliano , na kukutana na Warusi.

Ni wazi kwamba si rahisi kwa siku moja kuweza kupata suluhisho la mzozo huo wa mashariki ya kati , lakini ni hatua ndogo ya kuwezesha kupata eneo la kupitisha mahitaji ya kiutu pamoja na usitishaji wa mapigano, ili kuweza kuwapatia wakaazi wa Aleppo mahitaji muhimu kama chakula na madawa pamoja na maeneo mengine ya vita.

Na gazeti la Frankfurt Allgemeine Zeitung kuhusu kushambuliwa kwa msafara wa magari yaliyobeba misaada ya Umoja wa Mataifa linaandika:

Putin ni baba mlenzi wa Assad. Msaada wa kijeshi wa Urusi , pamoja na Iran hali ambayo imejiimarisha, kuuvunja si jambo tena la kujadiliwa. Ndege za Urusi na Syria zinashambulia, maeneo ya waasi , lakini mara chache maeneo yale ya wapiganaji wa Jihadi, lakini kila mara wanashambulia hospitali pamoja na maeneo ya misaada ya kiutu. Mabomu ya Urusi yameshambulia pia msafara wa malori ya misaada ya Umoja wa Mataifa baada ya kufuatilia ndege isoyokuwa na rubani ya Urusi. Serikali ya Marekani imetoa shutuma hizi , lakini Urusi inapinga hilo. Bila shaka kwa kuwa kuna suala la uhalifu wa kivita , iwapo itabainika kwamba wao ndio walioshambulia msafara huo wa malori ya misaada. Assad mmiliki wa mabomu ya mapipa na gesi ya sumu hatambui kabisa hilo.

Hata hivyo hana haja ya kuzuwia mashambulizi ya jeshi lake, na pia kupata suluhisho la kisiasa katika mzozo wa nchi yake.

Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Iddi Ssessanga