1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Clinton aendelee au asalim amri

23 Aprili 2008

Katika uchaguzi wa jana kuteua watetezi wa chama cha Democrat kwa uchaguzi wa rais,bibi Hilary Clinton ameshinda.

https://p.dw.com/p/DnDK
Barack Obama akipewa pole na mkewePicha: AP

Kwa kura 55 kwa 45 % za Barack Obama, seneta Hilary Clinton ameshinda jana uchaguzi wa kumteua mtetezi wa wadhifa wa rais wa mkoa wa Pennsylvania kwa chama cha Democrat.

Ushindi wake ukitarajiwa hatahivyo na macho yote yakikodolewa mwanya kati yake na Obama,mpinzani wake chamani.

Ilikua ashinde si kwa chini ya 10 % zaidi kumpita Obama , ndipo Bibi Hilary Clinton apewe nafasi ya kuendelea na kampeni-kwa muujibu wa wachunguzi wengi.

Kinyan'ganyiro cha kuania nani anateuliwa na chama cha Democrat kugombea wadhifa wa urais nchini Marekani,kimebakia kama hapo kabla kigumu kwakila Obama anaongoza kwa kuwa na wajumbe wengi na hata ushindi wa Hilary mkoani Pennsylvania ,haujabadili ukweli huo.Yamkinika pia hata mwisdhoni mwa chaguzi hizi za kwanza za kuteua watetzezi,bibi Hilary hataweza kumpita Obama kwa kura.Lakini hii haina maana,analaszimika kujitoa katika mbio hizi za kuania urais.Isipokua ameishiwa na fedha za kampeni.Lakini, ajitoe tu kwa kuwa anahisi hana nafasi ,itakua si tabia wala desturi ya kimarekani.Hapa kinachohesabiwa sio tu kushinda, bali pia kupigana hadi mwisho.

Isitoshe, utaratibu huu mrefu wa uchaguzi una pia nafuu yake.Katika mikoa mingi,watu wanatambua na kutanabahi kwamba kura zao si garasa bali zina turufu na uzito.Wanaitikia kwa kujipanga kwa wingi mistari kupiga kura .Chama cha Democrat kwahivyo, kinabidi kuwabakisha wapigakura hawa wapya kilichojipatia. Lakini pia shauku ya wafuasi wao kuibakisha hadi uchaguzi halisi wa urais hapo Novemba mwaka huu.

Kwani, ushindi wa mtetezi wa chama cha democrat dhidi ya mtetezi wa chama-tawala cha Republican-John McCain hauna uhakika hivyo.Isitoshe, yeyote kati ya watetezi hawa 2- Clinton na Obama, atahitaji kura za wafuasi wa mwenzake ili kushinda.Lakini wafuasi hao hawatakua tayari kumpigia kura mtetezi wa mpinzani wao ,endapo wakihisi wamehadaiwa kwavile, mtetezi wao waliemtaka alilazimishwa kumpisha mwenzake.

Au kwa kuwa wajumbe wenye kura za turufu-super-delegates-wamempokonya mtetezi wao nafasi ya ushindi.Au kwa kuwa kanuni za uteuzi zimebadilishwa kati kati ya uchaguzi na kwamba wajumbe wa mikoa ya Florida na Michigan kinyume na ilivyoafikiwa kabla,wanaruhusiwa kutoa sauti zao na kuhesabiwa.

Halkadhalika ,heshima ya kila mtetezi kwa mwenzake yafaa kutiwa maanani badala ya kubomoana.Katika timu ya kampeni ya Barck Obama,yasemekana inazingatiwa sasa ,kubadili mkondo wa kampeni na kuanza kumbomoa zaidi kwa njia chafu seneta Clinton .Kwani, timu ya kampeni ya bibi Clinton kwa kutumia njia hizo chafu kumbomoa Obama imefanikiwa. Lakini kufanya hivyo, kutampotezea Obama uadilifu na uaminifu.

Obama amewavutia wengi na kujipatia heba zaidi kuliko wanasiasa wengine kwa kuwa hajajitolea kushinda kwa kila hali.la hasha.

Na kwavile ,hataki kumuonea mpinzani wake ,yafaa afuate uizi huo huo.