1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Amri ya kuchunguza mauaji ya mwanasheria wa Kitamil

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtt

Rais wa Sri Lanka,Mahinda Rajapaksa,ametoa amri ya kuchunguza mauaji ya mwanasheria mashuhuri wa Kitamil aliepigwa risasi mjini Colombo alipokuwa njiani kwenda kazini.Chama cha kisiasa cha Watamil TNA,kimeiilaumu serikali kwa mauaji hayo kikisema kuwa hiyo ni juhudi ya kuwazima wafuasi wa chama hicho.Zaidi ya raia,wanajeshi na waasi 2,000,wameuawa katika machafuko yaliyoongezeka mwaka huu nchini Sri Lanka.Umoja wa Mataifa umelaani shambulio la juma hili lililofanywa na wanajeshi wa serikali kwenye kituo cha wakimbizi. Hadi watu 65 waliuawa katika shambulio hilo. Wakati huo huo,mratibu wa misaada wa Umoja wa Mataifa,Jan Egeland amesema,kuna habari zingine pia zinazotia wasi wasi kuwa waasi wamewazuia raia waliotaka kukimbia maeneo ya mapigano.