1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Mapambano makali kati ya vikosi na Tamil Tigers

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtP

Nchini Sri Lanka,mwanajeshi mmoja na hadi waasi 30 wameuawa katika mapambano yaliyozuka kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa Tamil Tigers,mashariki ya nchi hiyo.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi,wakati wa mapigano hayo katika wilaya ya Batticaloa,kambi nne za waasi pia ziliteketezwa.Tangu majuma kadhaa,mapigano makali yanaendelea katika eneo hilo la mashariki.