1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Tamil Tigers waua wanajeshi wa serikali, Sri Lanka

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByq

Wanamgambo wa Tamil Tigers wameshambulia kituo cha wanamaji wa Sri Lanka kaskazini mwa nchi hiyo na kuwaua wanamaji kadha.

Wanamgambo hao wamedai waliwaua wanamaji thelathini na watano kwenye shambulio hilo lakini majeshi ya Sri Lanka yamekanusha habari hiyo na yamesema wanamaji wasiozidi kumi ndio waliouawa.

Wakati huo huo, wanajeshi wawili wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada shambulio la bomu la kutegwa barabarani dhidi ya basi lilokuwa limebeba wanajeshi karibu na bandari ya Colombo.

Mapigano sasa yameelekezwa katika eneo la kaskazini la nchi hiyo tangu majeshi yalipoteka eneo la mashariki lililokuwa ngome ya wapiganaji wa Tamil Tigers.