1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Waasi 23 wa Tamil Tigers wauwawa

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBK3

Wanajeshi wa Sri Linka wamewaua waasi 23 wa kundi la Tamil Tigers katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Sri Lanka amesema mwanajeshi mmoja ameuwawa kwenye mapigano makali kati ya jeshi na waasi wa Tamil Tigers.

Waasi hao wanataka taifa huru la Tamil katika eno la kaskazini na mashariki mwa Sri Lanka.

Zaidi ya watu 70,000 wameuwawa tangu mgogoro huo ulipoanza mnamo mwaka wa 1983.