1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Wanafunzi watekwa nyara

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCi5

Waasi wa Tamil Tigers wamewateka nyara wanafunzi 24 katika eneo linalokabiliwa na hali ya wasiwasi la mashariki mwa Sri Lanka.

Polisi wamesema waasi hao wa,liwachukua watoto walio na umri kati ya miaka 15 na 17 na walimu wawili kutoka darasani mwao katika kijiji cha pwani Jumatatu jioni.

Waasi wa Tamil Tigers wamekanusha madai ya kuhusika na utekaji nyara huo.