1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombo.Mapigano yazuka tena upya kati ya waasi na vikosi vya serikali.

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxm

Siku moja baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya amani ya mjini Geneva, waasi wa Kitamil na vikosi vya kijeshi vya Sri Lanka wameshambuliana kwa silaha kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ulinzi ya Sri Lanka Brigedia Prasad Samarasinghe, waasi walianza kushambulia na kuwajeruhi wanajeshi watano jana, ndipo pande mbili hizo zilipoanza kujibizana mashambulizi ya silaha.

Nae msemaji wa waasi Daya Master, amelilaumu jeshi la serikali kwa kuaza mashambulizi ya hapo jana.

Mazungumzo ya amani nchini Switzerland kati ya waasi wa Kitamil na serikali ya Sri Lanka yalifeli hapo jana baada ya serikali kukataa matakwa ya waasi ya kuifungua njia kuu ya kaskazini ambayo inaunganisha sehemu ya kaskazini yenye waasi wengi na sehemu ya bara.