1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombo.Mapigano yazuka upya huku mbunge akipigwa risasi.

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuE

Watu wasio julikana wamempiga risasi na kumuua mbunge wa jamii ndogo ya Watamil katika mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo.

Mbunge huyo alikuwa ni mwanachama wa chama cha Tamil National Allience kinachoelemea zaidi upande wa wanamgambo wa Kitamil.

Wakati huo huo katika eneo la kaskazini mashariki mapigano ya baharini yameripuka upya kati ya wanamaji wa serikali na waasi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi la wanamaji limezamisha meli mbili za wasi na kuzuia kama wanavyodai, shambulio la kujitolea muhanga katika bandari ya Tricomalee.