1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO.Mlipuko mkubwa wauwa watu 95 na kuwajeruhi wengine 150

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2D

Vyombo vya habari vimeripoti juu ya mlipuko mkubwa dhidi ya msafara wa magari ya jeshi la Sri Lanka uliotokea kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Takriban watu 95 wameuwawa na wengine 150 wamejeruhiwa baada ya shambulio hilo la kujitoa muhanga.

Polisi imefahamisha kuwa bomu lililotegwa ndani ya gari lililipuka katika kijiji cha Digampathana mahala ambapo jeshi la Sri Lanka lilikuwa linakutana kabla ya kuelekea katika mji jirani wa pwani wa Trincomalee.

Habari zaidi zinafahamisha kuwa mabasi 13 yaliharibiwa vibaya katika mlipuko huo.

Wawakilishi wa serikali ya Sri Lanka wamelilaumu kundi la waasi wa Tamil Tigers kwa shambulio hilo.

Shambulio hilo limetokea wakati balozi wa amani wa Japan yupo mjini Colombo kwa mazungumzo na serikali ya Sri Lanka.