1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombo.Serikali yakubali kuifungua bara bara inayounganisha sehemu ya waasi.

31 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxQ

Serikali ya Sri Lanka imesema, ipo tayari kuifungua bara bara ambayo inaunganisha maeneo yanayoshikiliwa na waasi huko kaskazini pamoja na maeneo ya bara.

Kufunguliwa kwa njia hiyo kunatokana na kuvunjika kwa mazungumzo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Geneva, yaliyokuwa na lengo la kuokoa makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwaka 2002.

Waasi wa Kitamil na vikosi vya kijeshi vya serikali ya Sri Lanka, hapo jana walirushiana risasi katika maeneo yanayokaliwa na waasi.

Wakati huo huo wawakilishi wa chama cha Watamil (LTTE) wameakhirisha mpango wao wa kuitembelea Norway na Iceland, na kusema kuwa watarejea Sri Lanka kwa ajili ya mapambano.