1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombo.Waasi washambulia jeshi la serikali.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5E

Zaidi ya wapiganaji 50 wameuwawa katika mapigano makali kati ya majeshi ya serikali na waasi wa Tamil Tigers mashariki mwa Sri Lanka.

Maafisa wa kijeshi wa Sri Lanka wamesema waasi wa Tamil Tigers wamefanya shambulio katika kituo cha kijeshi katika eneo la Mankerni katika wilaya Batticaloa mapema jana Ijumaa.

Jeshi hilo likisaidiwa na helikopta za kijeshi, limerejesha mashambulizi hayo ya waasi, lakini mapambano yaliendelea kwa siku nzima.