1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONACKRY : Serikali yazungumza na vyama vya wafanyakazi

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRr

Serikali ya Guinea hapo jana imefanya mazungumzo na vyama vya wafanyakazi vinavyohusika na fujo ambazo zimepelekea kutangazwa kutumika kwa sheria ya kijeshi nchini humo huku kukiwa na onyo kwamba nchi hiyo inaweza kutumbukia kwenye machafuko.

Vyama vya wafanyakazi wiki hii vilianza tena maandamano mapya dhidi ya utawala wa Rais Lansana Conte ambapo wakati wa siku mbili za mgomo wa taifa rais huyo ameamuru sheria ya kijeshi kutumika nchini kote.

Mtu mmoja zaidi ameuwawa katika mji wa mkoani hapo jana na kufanya idadi ya watu waliouwawa na wanajeshi kwa kukaidi masharti makali ya sheria ya kijeshi kufikia tisa sheria ambapo kwayo wanajeshi wamepewa amri ya kufyatuwa risasi wakati wakikabiliwa na upinzani au na tishio la kushambuliwa.

Mazungumzo hayo yalioitishwa na spika wa bunge Aboubakar Sompare yanahudhuriwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wawakilishi wa kijeshi,viongozi wa dini na wa biashara.