1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY: Guinea yaregeza marufuku ya kutotembea nje

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQq

Guinea imeregeza sheria ya kutotembea nje huku maandamano ya kupinga utawala wa miaka 23 wa rais Lansana Conté yakipungua.

Kiongozi wa utumishi katika jeshi la Guinea, kamanda Kerfalla Camara, amesema kuanzia leo Jumatatu wananchi watakuwa na uhuru wa kutembea nje kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.

Guinea ilitangaza hali ya hatari mnamo Jumatatu iliyopita ili kukabiliana na wimbi la maandamano ya machafuko na mgomo wa kitaifa ambapo watu zaidi ya 100 waliuwawa.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanataka rais Conté ajiuzulu. Viongozi wa upinzani wanasema mamia ya watu wametiwa mbaroni na polisi tangu hali ya hatari ilipotangazwa nchini Guinea.