1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY: Mgomo wasimamishwa nchini Guinea baada ya maridhiano kati ya pande husika..

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXA

Vyama vya wafanyikazi nchini Guinea vimesimamisha mgomo uliokuwa ukiendelea baada ya kuafikiana na serikali ya Lansana Conte imteue waziri mkuu na pia ipunguze bei ya mafuta na mchele.

Wakati wa mgomo huo ulioendelea kwa siku kumi na nane, makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama yalisababisha vifo vya watu hamsini na tisa.

Rais Lansana Conte ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka elfu moja mia tisa na themanini na nne, anakabiliwa na upinzani kwa sababu ya ukosefu wa ajira na pia mfumko wa bei.