1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY:Gaddafi aulaumu umoja wa sasa wa Afrika

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnw

Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi amesema kuwa umoja wa sasa wa Afrika umeshindwa kuwajibika na kwamba suluhisho pekee ni kuwa na serikali moja ya Afrika.

Akizungumza katika mji mkuu wa Guinea Conakry, Kanali Gaddafi amesema kuwa hakuna majaaliwa iwapo afrika itaendelea kuwa kama ilivyo hivi sasa.

Amewataka viongozi wa kiafrika wanaotarajiwa kudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika mwezi ujayo nchini Ghana kuamua kuanzisha Shirikisho la Nchi za Afrika.

Gaddafi kwa muda mrefu amekuwa akipigia upatu mawazo hayo ambayo baadhi ya wadadisi wanasema kuwa hayatekelezeki.

Kanali Gaddafi alifanya ziara pia nchini Sierra Leone ambapo katika mji mkuu wa Freetown maelfu ya watu walijipanga barabarani kumlaki, pamoja na tuhuma ya kwamba alikuwa akiliunga mkono kundi katili la RUF: