1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Condoleeza Rice awasili Kenya

Mtullya, Abdu Said18 Februari 2008

Condoleeza Rice awasili Kenya.

https://p.dw.com/p/D908



NAIROBI:

Waziri wa wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice anatarajiwa kukutana na rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Waziri huyo pia atafanya mazungumzo na aliekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ambae kwa sasa anaongoza mazungumzo ya kuleta suluhisho la mgogoro wa kisiasa nchini Kenya.

Waziri huyo wa Marekani anawasili Kenya wakati ambapo waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Moses Wetangula ameshaeleza wazi kuwa tatizo la Kenya litatatuliwa na watu wa nchi hiyo.