1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Condoleezza Rice asema hali nchini Kenya inatia wasiwasi

30 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CzXb

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, amesema machafuko yanayoendelea nchini Kenya yanatia wasiwasi.

Kwa mara nyingine kiongozi huyo amewataka viongozi wa Kenya watafute suluhisho la kisiasa kwa mzozo uliosababishwa na matokeo ya uchaguzi wa tarehe 27 mwezi Disemba mwaka jana.

Condoleezza Rice amewaambia waandishi wa habari mjini Washington kwamba kuna haja ya kila mkenya kuwa na utulivu na kuziunga mkono juhudi za Kofi Annan kutafuta makubaliano kati ya rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Condoleeza Rice ambaye alikuwa akikutana na waziri wa mashauri ya kigeni wa Albania, Lulzim Basha, kujadili maswala mengine, amesema atawasiliana na Kofi Annan hii leo kutathmini vipi Marekani na nchi nyingine zinavyoweza kusaidia kuumaliza mzozo huo wa kisiasa nchini Kenya.