1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congo yatangaza mkutano wa amani wa Kivu

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cd0O

KINSHASA

Maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hapo jana wametangaza kwamba watakuwa na mkutano wa amani mwishoni mwa mwezi wa mwezi huu katika jimbo la machafuko mashariki mwa nchi hiyo baada ya kuhasirika katika mapigano ya hivi karibuni na waasi.

Spika wa bunge na mbunge wa mkoa wa Kivu Kusini Vital Kamere amesema mkutano huo wa siku tisa unaotazamiwa kuanza hapo tarehe 27 mwezi wa Desemba unaandaliwa na Rais Laurent Kabila kwa lengo la kukomesha vita na kuanzisha msingi wa amani ya kudumu.

Mkutano huo utahudhuriwa na wawakilishi wa raia,viongozi wa biashara na makundi ya kikabila lakini haijulikani iwapo waasi pia watajumuishwa kwenye mkutano huo.