1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COPENHAGEN: Machafuko mapya yazuka

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNJ

Machafuko mapya yamezuka tena mjini Copenhagen nchini Danmark huku waandamanaji wakichoma moto magari na kupambana na polisi.

Machafuko hayo yanafanyika siku moja baada ya polisi kuwakamata waandamanaji takriban 220 waliowarushia mawe, chupa na rangi wakati kikosi cha polisi kilipowafukuza watu wasio na ardhi kutoka kwa jumba la maonyesho ya michezo.

Mwanamume mmoja raia wa Ujerumani alijeruhiwa wakati wa machafuko hayo huku wajerumani tisa wakiwa miongoni mwa waliokamatwa na polisi.

Jumba hilo la maonyesho limekuwa likitumiwa kama makaazi ya raia kwa miaka mingi. Hata hivyo shirika la kanisa lililolinunua jengo hilo mnamo mwaka wa 2000, lilipewa kibali na mahakama cha kuwafukuza watu waliokuwa wakiishi humo, kilichopuuzwa.