1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COPENHAGEN: Waandamanaji watetea wavamiaji nyumba

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMv

Askari polisi nchini Denmark wametumia gesi ya kutoa machozi kuvunja maandamano ya kama vijana 1,000 wanaopinga hatua ya kuwafukuza wavamiaji nyumba,katika mji mkuu Copenhagen.Waandamanaji kwa usiku wa tatu kwa mfululizo wameandamana,huku wengine wakirusha mawe na mabomu ya mkono ya kienyeji na magari mengi yalitiwa moto.Si chini ya watu 150 wamekamatwa,lakini msemaji wa polisi hakuweza kuthibitisha ripoti zilizosema kuwa Wajerumani kadhaa ni miongoni mwa wale waliokamatwa.