1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cote d'Ivoire.

26 Desemba 2010

Raia 14,000 wa Cote d'Ivoire wakimbilia Liberia.

https://p.dw.com/p/zpnj
Wakaazi wa Cote d'Ivoire.Picha: picture alliance / dpa

Kiongozi aliyepo  madarakani  hivi  nchini  Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo, amekataa kwa kutaja kutokuwa haki, tishio la viongozi wa mataifa  ya  jumuiya ya  Afrika  magharibi  la kumuondoa kwa nguvu.

Elfenbeinküste Laurent Gbagbo Flash-Galerie
Laurent Gbagbo.Picha: picture-alliance/dpa

Ijumaa Viongozi wa jumuiya ya kibiashara ya mataifa ya  Afrika  magharibi , ECOWAS walionya kwamba iwapo Gbagbo hatompisha mpinzani wake Alassane Outtara, basi  hawataondoa  uwezekano  wa  kutumia  nguvu. Hilo lilikuwa tishio la kwanza la moja kwa moja la kuingiliakati  kijeshi, la  mataifa ya nje katika mkwamo huo wa uchaguzi, ambao kiasi ya watu 200 wameuwawa.

Umoja wa mataifa, Umoja wa Afrika, na ECOWAS, zote zimetambua matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yaliyoonyesha  kuwa Outtara  ndie mshindi wa uchaguzi huo wa Novemba. Wakati huo huo kiasi ya watu 14,000 wamekimbia nchini Cote d'Ivoire kuelekea nchi jirani ya Liberia, kutokana na wasiwasi kwamba mzozo huo wa uchaguzi utazusha mapigano ya ndani.

Mwandishi Maryam Abdalla/RTRE

Mhariri:Sekione Kitojo.