1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cote d'ivoire

Abdu Said Mtullya31 Desemba 2010

Mgogoro wa kisiasa nchini Cote d'ivoire umo katika hatari ya kuwa mkubwa zaidi.

https://p.dw.com/p/zroE
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika doria mjini AbidjanPicha: AP

Mgogoro wa kisiasa nchini Cote d'ivoire umo katika hatari ya kuwa mkubwa zaidi baada ya waziri wa vijana kutoa mwito kwa wafuasi wa rais Gbagbo wa kuiteka hoteli ambapo kiongozi wa upinzani Alassane Outtara kwa sasa anakaa.Hoteli hiyo iliyopo katika mji mkuu wa Cote d'ivoire,Abidjan inalindwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -Moon ameonya dhidi ya kuishambulia hoteli hiyo.Msemaji wake ameeleza kuwa askari wa Umoja wa Mataifa wamepewa jukumu la kuwalinda viongozi wote waliomo ndani ya hoteli hiyo.

Umoja wa Mataifa pia umedai kwamba wanajeshi wanaomtii rais Gbagbo wanaizuia njia ya kuendea kwenye makaburi ya watu wengi waliozikwa pamoja.Pana tuhuma kwamba maiti hadi 80 zimezikwa katika jengo moja.Ghasia zilizotokea baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa zimesababisha vifo vya watu zaidi ya 170.