1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cote d'Ivoire.

2 Januari 2011

Ban Ki Moon akariri kumuunga mkono Alassane Ouattara.

https://p.dw.com/p/zsY7
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha: AP

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon kwa mara nyingine tena amesema kuwa anamuunga  mkono  Alassane Outtara kiongozi wa Cote d'Ivoire anaetambulika kimataifa.

Rais Laurent Gbagbo mpaka sasa amekataa kuyakubali matokeo ya uchgauzi wa hivi karibuni na kuondoka madarakani. Mzozo huo umezusha ghasia katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Laurent Gbagbo / Elfenbeinküste / Abidjan
Kiongozi wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo.Picha: AP

Katika mazungumzo ya simu, Ban alimueleza Outtara kwamba vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vimeamrishwa kufanya kila kiwezekanacho ili kuweza kuingia maeneo ambako inatuhumiwa kuwa maiti nyingi zimezikwa pamoja.

Kambi ya Outtara imewalaumu wafuasi wa Gbagbo kwa mauaji ya wafuasi wake.