1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CPJ yaitaka Tanzania kumuachia huru mchora katuni John Fwema

8 Oktoba 2021

Kamati ya Kuwatetea Waandishi wa Habari, CPJ, imeitaka Tanzania kumuachia huru mchora katuni John Fwema na kuachana na uchunguzi wa waandishi wengine wawili wa televisheni ya mtandaoni, Harold Shemsanga, na Ernest Mgawe.

https://p.dw.com/p/41S7w
Cartoon Toonpool | Commander in chief

Tarehe 24 Septemba polisi ilimkamata Fwema nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na hadi leo imemzuia katika kituo cha polisi cha Oysterbay, kwa mujibu wa Muungano wa Watetezi wa Binadamu Tanzania, THRDC, na kaka yake Fwema, Florence Fwema.

Polisi inasema Fwena anachunguzwa kwa makosa ya mtandaoni lakini bado haijamfikisha mahakamani.

Fwema alikamatwa siku kadhaa baada kuweka katuni katika ukurasa wake wa Instagram iliyoonekana kumkosoa Rais Samia Suluhu Hassan

Kando na tukio hilo, mnamo Oktoba 2 polisi ilimkamata  Shemsanga mmiliki wa televisheni ya mtandaoni ya Mgawe wakati akifuatilia ripoti ya wanachama wa Baraza la Wanawake la chama cha upinzani cha CHADEMA na baadaye kuachiwa huru lakini polisi bado wanamchunguza kwa kukusanyika kinyume cha sheria.