1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CUF yamfukuza Hamad Rashid na wenzake

Othman Miraji4 Januari 2012

Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania limeamua kwa wingi wa kura kumfukuza mmoja wa waasisi wa chama hicho na mwanasiasa mkongwe, mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed, na wenzake watatu.

https://p.dw.com/p/13dqx
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad.
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad.Picha: DW

Wanachama hao wakiongozwa na Rashid wametiwa hatiani na Baraza hilo kwa kuendesha njama za kukivuruga chama hicho. Othman Miraji amezungumza kwa njia ya simu na mwakilishi wa mji mkongwe wa Zanzibar ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF kwa upande wa Zanzibar, Ismail Jussa, kuhusiana na yaliyojiri kwenye kikao hicho.

Mwandishi: Othman Miraji
Mhariri: Saumu Mwasimba