1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR : Afrika Magharibi yahitaji msaada dola milioni 309

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmA

Umoja wa Mataifa umetowa wito hapo jana wa msaada wa kibinadaamu wa thamani ya dola milioni 309 hapo mwakani kwa nchi 16 za Afrika Magharibi baadhi yao zikiwa ni miongoni mwa nchi fukara kabisa duniani.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema fedha hizo zinahitajika kushughulikia uhaba wa chakula,maji ya kunywa, madawa na kutibu dhuluma za ngono hususan kwenye eneo kavu la Saghel kusini tu kidogo mwa Sahara.

Kila mwaka takriban watoto 300,00 wenye umri wa chini ya miaka mitano hufariki kutokana na utapia mlo katika eneo hilo ambalo linakabiliwa na ukame mbaya kabisa kuwahi kushuhudiwa katika historia.

Watu milioni 250 wanaishi Afrika Magharibi.Umoja wa Mataifa unasema watoto nchini Burkina Faso,Chad,Mali, Mauritania na Niger wataathirika zaidi kutokana na utapia mlo.