1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR: Idadi ya vifo vya watoto duniani yashtusha

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtn

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto duniani-UNICEF limesema,idadi kubwa ya vifo vya watoto vinavyotokea barani Afrika inashtua sana.Mkurugenzi wa shirika hilo,Bibi Ann Veneman amesema,nusu ya watoto milioni 10 wanaofariki kila mwaka kote duniani kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiliwa pamoja na utapiamlo,hufariki katika nchi za Kiafrika.Bibi Veneman amekuwa ziarani Senegal ambako uchunguzi uliofanywa na serikali huonyesha kuwa tangu mwaka 2002,idadi ya vifo vya watoto nchini humo imepunguka kwa asilimia 15.