1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR : Vita vyakwamisha maendeleo Afrika

11 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gk

Utafiti mpya umeonyesha kwamba vita vya wenywewe kwa wenyewe na mizozo vimeligharimu bara la Afrika zaidi ya euro bilioni 200 kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2005.

Utafiti huo unadai kwamba kima hicho ni sawa na michango ya fedha iliotolewa kwa bara hilo katika misaada ya kimataifa katika kipindi kama hicho.

Utafiti huo uliofanywa na mashirika matatu yasio ya kiserikali ni wa kwanza kujaribu kuweka takwimu juu ya athari za mizozo kwa maendeleo barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni.

Katika dibaji ya repoti hiyo Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametowa wito kwa Afrika na dunia kushirikiana kuwa na mkataba wa biashara ya silaha ambao utakomesha mmiminiko wa silaha barani humo.