1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR : Wasenegali wapiga kura leo

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOq

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal anakusudia kunyakua ushindi leo hii katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo lakini wapinzani wakiwemo washirika wake wa zamani wameapa kupinga uhalali wa ushindi wowote ule wa mwanasiasa huyo mkongwe utakaopatikana moja kwa moja katika dura ya kwanza ya uchaguzi.

Wade amewaambia wafuasi wake katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni hapo Ijumaa kwamba ana hakika kusomba zaidi ya asilimia 50 ya kura akimaanisha kwamba hakutakuwa na haja ya kuwepo kwa duru ya pili ya uchaguzi.

Baadhi ya wagombea 14 wanaotarajia kumuenguwa wameonya hadharani kwamba watapinga matokeo hayo kuwa ya udanganyifu iwapo Wade atashinda moja kwa moja kwenye duru hiyo ya kwanza.

Wade alichaguliwa kuwa rais hapo mwaka 2000 na kukomesha miongo minne ya utawala wa kisoshalisti.Kampeni yake imejumuisha ahadi za miradi ya kutowa ajira ya kujenga mabarabara makubwa, hoteli zenye hadhi ya nyota tano,reli nna viwanja vya ndege katika jaribio la kuzuwiya uhamiaji mkubwa wa vijana wanaojaribu kukimbilia Ulaya katika miaka ya hivi karibuni.