1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR.Matokeo ya uchaguzi bado yanasubiriwa

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOG

Waziri mkuu wa Senegal Macky Sall amedai kuwa rais Abdoulaye Wade aliyepambana na wagombea 14 katika uchaguzi wa rais wa siku ya jumapili ameshinda kwa asilimia 57.

Tamko hilo la Sall ambae pia ni meneja wa kampeni ya rais Abdoulaye Wade limepingwa vikali na watetezi wa upande wa upinzani.

Hata hivyo matokeo rasmi bado hayajatangazwa.

Takriban raia milioni tano wa Senegal walijitokeza kupiga kura na kusababisha vituo vibakie wazi hata baada muda wa kupiga kura uliopangwa kumalizika ili kukidhi idadi kubwa ya watu.