1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR.Rais Abdoulaye Wade atarajiwa kunyakua ushindi

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOM

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal anatarajiwa kushinda kipindi kingine cha miaka mitano katika uchaguzi nchini humo.

Taarifa za matokeo ya awali katika uchaguzi huo wa urais yanaonyesha kuwa rais Wade anaongoza.

Rais Abdoulaye Wade alipambana na wagomea wengine 14 katika kinyang’anyiro hicho ana imani kwamba atashinda kwa asilimia 50 kiwango kinacho takiwa ili kuweza kuendelea kuingoza Senegal.

Uchaguzi huo wa urais nchini Senegal umeshuhudiwa na mamia ya wasimamizi wa uchaguzi wa kimataifa.