1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR:Upinzani kususia uchaguzi wa wabunge

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBw4

Senegal inafanya uchaguzi wa wabunge mwishoni mwa juma huku upinzani ukitisha kususia.Hatua hiyo inatokea miezi mitatu baada ya Rais Abdoulaye Wade kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa rais hata baada ya upinzani kudai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na hila.Nchi ya Senegal inaelezwa kama mfano mzuri wa demokrasia barani Afrika.

Hatua ya vyama 17 kususia uchaguzi huo itaipa muungano wa chama tawala cha PDS na vyama vinayomuunga mkono Rais Wade ushindi wa rahisi.

Vigogo wa upinzani wakiwemo Waziri mkuu wa zamani Idrissa Seck na Ousmane Tanor Dieng wa chama tawala cha zamani cha Socialist hawatahusika katika uchaguzi huo.Viongozi hao walichukua nafasi za pili na tatu katika uchaguzi wa rais uliopita.

Upinzani uliamua kususia uchaguzi huo baad ya Rais Wade kukataa kufanya mabadiliko katika sheria za uchaguzi.

Zaidi ya wagombea alfu 4 wanawania nafasi 150 bungeni.