1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria iko tayari kufufua mazungumzo ya amani na Israel

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCW

Spika wa bunge la Marekani bibi Nancy Pelosi amesema kwamba rais Bashar al-Assad wa Syria amemueleza kwamba Damascus iko tayari kuanzisha tena mazungumzo ya amani na Israel.

Akizungumza na wandishi wa habari mjini Damascus, bibi Pelosi amesema kuwa aliwasilisha ujumbe kama huo kwa rais Assad kutoka kwa waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert.

Bibi Pelosi amesema ametumia nafasi ya kukutana kwake na kiongozi wa Syria kueleza wasiwasi wa Marekani kuhusu kuingia nchini Irak wapiganaji wenye msimamo mkali kupitia Syria na pia juu ya Syria kufadhili makundi ya wanamgambo ya Hamas na Hezbollah.

Rais George W Bush wa Marekani amekosoa ziara hiyo ya bibi Pelosi, amesema kuwa ziara hiyo imepeleka ujumbe usio sahihi kwa Syria.