1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria yasema madai ya Marekani ni kichekesho

2 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwj

Syria imekanusha madai ya Marekani kuwa imepanga njama pamoja na Iran na Hezbollah kuipindua serikali ya Lebanon.Ubalozi wa Syria mjini Washington umesema madai hayo ni “kichekesho.” Hapo awali msemaji wa Ikulu ya Marekani Tony Snow alisema kuna ushahidi kuhusiana na njama hiyo.Azma mojawapo ya Syria ni kuzuia kuundwa mahakama ya kimataifa kuchunguza mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri aliongezea Tony Snow.Inasemekana kuwa idara ya upelelezi ya Syria pia ilikuwa na mkono wake katika mauaji hayo.